Friday, 20 April 2012

Garisa yafaidi ukuaji wa mali isiyohamishika

Na Bosire Boniface, Wajir

Aprili 18, 2012
Wawekezaji waliokimbia Kaskazini Mashariki mwa Kenya kutokana na ongezeko la kutokuwepo usalama miaka ya 90 sasa wanarejea kushiriki katika maendeleo, maafisa na wachambuzi wasema.
  • Majengo mapya yamejengwa hivi karibuni huko Ngamia Road mjini Garisa. Uimarishaji wa usalama umeongeza hamu ya maendeleo Kaskazini Mashariki mwa Kenya. [Bosire Boniface/Sabahi] Majengo mapya yamejengwa hivi karibuni huko Ngamia Road mjini Garisa. Uimarishaji wa usalama umeongeza hamu ya maendeleo Kaskazini Mashariki mwa Kenya. [Bosire Boniface/Sabahi]
"Eneo hili lilikumbwa na hofu na wasiwasi kwa sababu ya taarifa za kukosekana kwa usalama. Watu wengi waliuawa na biashara kushambuliwa," alisema Siyat Abdi Hussein, mwendelezaji wa mali isiyohamishika na mshauri.
"Mwanzoni mwa miaka ya 60, Wilaya za Northern Frontier, sasa inayojumuisha majimbo ya Garissa, Mandera, Wajir, Marsabit na Isiolo, zilitaka kujitenga na kujiunga na Jamhuri kubwa ya Somalia. Vita vya kujitenga viliwapa njia kwa majambazi ambao waliutikisa mkoa kwa hofu, kuua mamia ya watu na kuwalemaza wengi zaidi, " Hussein aliiambia Sabahi.
"Lakini kutokana na miundo ya usalama na ya kijamii, majambazi wenye silaha ambao walisusurika mkoa huu hadi mwanzo mwa miaka ya 2000, hayapo tena," alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Mashariki James ole Seriani aliiambia Sabahi kuwa eneo hilo ambalo lilijaja vibanda, sasa lina majengo marefu.
Alisema kuwa mashambulizi ya karibuni ya al-Shabaab ya mabomu ya kuzika ardhini na maguruneti katika eneo hili, hayatazuia uongezekaji wa mali.
"Daima hatukuwa tunavutia watalii, lakini kwa miaka michache iliyopita, licha ya vitisho vya al-Shabaab, tumeandikisha idadi ya watalii wanaokuja katika eneo hili kwa ajili ya biashara na burudani," Seriani alisema.

'Fedha haramu’ hazikaribishwi

Seriani alisema serikali kukaribisha maslahi mpya mkoa humo kumesababisha kuongezeka kwa wawekezaji, lakini uwekezaji haramu hautavumiliwa. Viongozi wahakikisha kuwa ongezeko la mali haliwi njia ya maharamia kuhaulisha fedha, alisema.
"Garissa ni lango kuu la Kaskazini Mashariki mwa Kenya na Pembe ya Afrika, linaloifanya kuwa ni sehemu ya mavuno katika masuala ya biashara na maendeleo. Lakini kadiri kanda hii itakavyokuwa muafaka kwa uwekezaji, hatutaruhusu fedha haramu kutoa mchango katika maendeleo hayo," Seriani alisema.
Mshauri wa uwekezaji na maendeleo Ibrahim Ahmed Rashid aliiambia Sabahi kwamba zaidi ya miaka miwili iliyopita, mahitaji ya mali yameongezeka sana kiasi kwamba baadhi ya wawekezaji wapo tayari kulipa zaidi ya mara mbili kwa ajili ya kipande cha ardhi.
Wanunuzi wanakuja kutoka nje ya nchi pamoja na maeneo mengine ya Kenya, alisema, na kuongeza kuwa eneo la ofisi za biashara linahitajika sana mjini Garissa kiasi kwamba watu wanatafuta wajenzi hata kabla ya kuweka msingi.
"[Wawekezaji] wamekuwa wanalenga kupata ardhi ya kimkakati na kupendekeza bei za majaribu kwa wale ambao wanamiliki ardhi lakini hawana uwezo wa kuendeleza vipande yao," Ahmed alisema.
Lakini Ahmed alisema kuwa ongezeko hili changa pia limesababisha walanguzi wa mali, na alitoa wito wa tahadhari.
"Tunaona makampuni ya madalali wa ardhi na wajenzi wajanja," alisema. "Wekeza shilingi milioni 3 (sawa na dola za Kimarekani 37,500) katika kipande cha ardhi ambacho thamani yake rasmi ni shilingi 500,000 (sawa na dola za Kimarekani 6,250) bila ya kuwa na hati miliki kunaweza kusababisha machafuko," alisema.

Mahitaji makubwa mno ya ardhi

Viongozi wanaohusika na uwekezaji katika ardhi waliiambia Sabahi kwamba wanazidiwa na mahitaji ya kipekee ya ardhi, kwa kuzingatia kwamba kanda hapo nyuma ilikuwa eneo lililotengwa.
"Mara nyingi, inanibidi kuzima simu yangu ili niweze kulala," alisema Mohamud Ahmed Santur, karani katika Halmashauri ya Manispaa ya Garissa ambaye anashughulika na wawekezaji wa ardhi. "Hivi sasa kuna maslahi makubwa mno ya ardhi na hii imefikia kilele katika miaka mbili au mitatu iliyopita."
"Sehemu moja ya nane ya ekari sasa inauzwa kati ya shilingi milioni 2 na 3 (dola za Kimarekani 25,000 na 37,500), kutoka shilingi 200,000 (dola za Kimarekani 2,500) miaka minne tu iliyopita," alisema.
Minnie Wacuka, afisa katika Ofisi ya Msajili wa Ardhi Garissa, aliiambia Sabahi kwamba watu wamekuwa wakishiriki katika kununua ardhi bila ya kuangalia kwanza kama ardhi hiyo ipo kweli.
"Baadhi ya ardhi zilizowekewa uzio kama mali binafsi zimetengwa kwa madhumuni mengine, kama vile bustani za umma, na tumekuwa na migogoro ambapo kuna kufukuzwa kwa watu au mmiliki halisi anataka kuendeleza ardhi yake. Pia tulishuhudia kuzuka kwa mapigano ya koo inayosababishwa na migogoro ya ardhi, "alisema.
Afisa wa Ardhi Wilaya ya Garissa James Kemoni aliiambia Sabahi kuwa serikali imechukua hatua za kuzuia udanganyifu.
"Baadhi ya makampuni ya hapa huuza ardhi kwa wanunuzi wasiowatilia shaka, baadaye kuviuza tena viwanja hivyo hivyo kwa watu mbalimbali, bila serikali kutoa kibali cha uuzaji huo. Mtu yeyote anayetaka kununua ardhi hutakiwa kuthibitisha hali ya ardhi hiyo na sisi kabla ya kuondoka na fedha zao," alisema.
Meya wa Garissa, Ismail Mohammed Garat, aliiambia Sabahi kuwa kanda hii ina uwezo mkubwa. "Ndoto yetu ni kuwa [mji] wenye hadhi ulimwenguni kama Dubai," Garat alisema. "Katika miaka mitano ijayo, ndoto yetu ni kuwa na mji ambapo watu kutoka mkoa huu watasahau juu ya miji mingine."
Lakini alisema mji una njia ndefu ya kufikia huko.
Ongezeko hilo bado halijawa guswa wakazi ambao wanaishi katika vibanda vya udongo vinavyofunikwa na kivuli cha mabungalows ya gharama kubwa, nyumba za ranchi, maghorofa na nyumba za kifahari za familia mbili na familia tatu.
Mohammed Hussein Abdi, mwenye umri wa miaka 56 na mshona viatu wa Iftin, Garissa, aliiambia Sabahi kuwa hawezi kwenda sambamba na kasi ya ukuaji huo.
Garissa inaingia katika ustaarabu kwa haraka, Abdi alisema. "Ni nzuri, lakini baadhi yetu ambao hatuna pesa tumekuwa tukikanganywa na mabadiliko."

No comments:

Post a Comment