Tuesday 4 September 2012

Waandishi wa habari wa Somalia wavumilia katika taaluma yao licha ya hatari



Na Mahmoud Mohamed, Mogadishu

Agosti 31, 2012
Mwandishi wa habari wa Mogadishu Abdifatah Ahmed amepokea vitisho ya kifo mara kadhaa kutoka kwa wanamgambo katika miaka mitatu iliyopita.
  • Waandishi wa habari wa Somalia wakijipanga mbele ya makao makuu ya AMISOM, kusubiri kuandika juu ya sherehe za uapishaji wa wabunge wapya tarehe 20 Agosti. [Na Mahmoud Mohamed/Sabahi] Waandishi wa habari wa Somalia wakijipanga mbele ya makao makuu ya AMISOM, kusubiri kuandika juu ya sherehe za uapishaji wa wabunge wapya tarehe 20 Agosti. [Na Mahmoud Mohamed/Sabahi]
"Hata kama tunakuwa walengwa wa watu wenye msimamo mkali, hatutatishika na vitisho kama hivyo vya uwoga," aliiambia Sabahi.
Ahmed alisema amechukua hatua kadhaa za tahadhari tangu alipoanza kupokea vitisho.
"Baadhi ya hatua nilizochukua ni pamoja na kubadilisha kila mara njia yangu wakati ninaposafiri baina ya nyumbani na pahali pa kazi, pamoja na kubadilisha ratiba zangu za kila siku," alisema. Mara nyengine huamua kusafiri na walinzi."
Kwa waandishi wa habari nchini Somalia, 2012 imekuwa mwaka wa damu.
"Katika muda wa miezi minane ya kwanza ya mwaka huu, waandishi wa habari 9 wameuwawa na 20 wengine kujeruhiwa katika mikono ya watu wenye silaha, na kuufanya mwaka huu kuwa mbaya na wa damu zaidi kwa waandishi wa habari wa Somalia," alisema Abdullahi Mohamed Hassan, mkurugenzi wa Nyumba ya Vyombo vya Habari Mogadishu, ambayo inashughulikia kukuza amani na kulinda haki za waandishi wa habari.
Hivi karibuni zaidi, tarehe 12 Agosti, waandishi wa habari wa Somalia Yusuf Ali Osman na Mohamud Beneyste waliuliwa katika mikono ya watu wasiojulikana wenye silaha mjini Mogadishu.
Mohamed Ahmed, mwandishi wa habari mkongwe anayeishi Mogadishu na kufanya kazi kama mhariri wa tovuti ya habari nchini Somalia, alisema yeye pia amekuwa akitumiwa ujumbe za vitisho.
"Tangu mwaka 2009, nimepokea barua kadhaa na simu kutoka kwa watu nisiowajua wanaodai ni kutoka kikundi chenye msimamo mkali cha al-Shabaab na kutishia kuniua," aliiambia Sabahi. "Wanaweza kuniambia eti mimi ni adui wa Uislamu na kwamba, Mungu akipenda, mujahidina watanisaka na kunimaliza."
Ahmed alisema anaogopa kwa sababu wenzake wengi, ambao pia walikuwa wametishiwa, waliuwawa na watu wasiojulikana wenye silaha.
Hata hivyo, Ahmed alisema, "Sijawahi kufikiria kuiacha kazi yangu na kuikimbia nchi yangu. Kama ningekuwa wa kuacha kazi yangu kwa sababu ya vitisho vya kipuuzi kama hivyo, hii ingemaanisha kuwa wanamgambo wamefanikiwa malengo yao na kuvinyamazisha vyombo vya habari."
Abdiaziz Biilo, mwandishi wa habari wa Mogadishu wa Press TV, alisema kufanya kazi kama mwandishi wa habari nchini Somalia ni changamoto kubwa sana.
"Kila asubuhi, unaondoka nyumbani kwako na kwenda kazini bila ya kujua kama utarejea salama au la. Ni mazingira magumu sana na usalama hauhakikishwi kwa wale wanaofanyakazi katika vyombo vya habari," aliambia Sabahi.
"Nimehudhuria mazishi ya waandishi wa habari wenzangu kadhaa ambao walipigwa bunduki mjini Mogadishu na watu wasiojulikana. Kila siku huwa ninajiuliza, " Nani atafuatia?"
"Waandishi wa habari wa Somalia wanauliwa kwa sababu ya taaluma yao," alisema. Licha ya hayo, hatutaacha kazi yetu kwa kuwaogopa wanamgambo kwa sababu tunahisi tunawatumikia watu kwa kuwapatia habari na ukweli uliopo nyuma ya kile kinachotokea nchini."
Mohamed Abdullahi, mwandishi wa habari wa kujitegemea anayeishi Mogadishu, alisema, "Mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari wa Somalia daima hayatasita. Kuna vyombo vingi nyuma ya hili, lakini kikundi cha al-Shabaab chenye mafungamano na al-Qaida ndicho ni tishio kubwa la kwa waandishi wa habari."
"Al-Shabaab wanawachukulia waandishi wa habari kama maadui wao nambari moja kwa sababu [waandishi wa habari] wanaeneza ukweli na kufichua uhalifu wa kikatili unaofanywa dhidi ya raia na kikundi hiki kila siku," alisema.

http://sabahionline.com/sw/articles/hoa/articles/features/2012/08/31/feature-01?change_locale=true

No comments:

Post a Comment